Waziri Mkuu wa Australia Malcolm Turnbull ana tarajia kukumbwa na upinzani mkali toka kwa viongozi wa mikoa na majimbo kuhusu mipango ya serikali yaku badili jinsi mapato ya kodi ya bidhaa na huduma ama GST kama inavyo julikana hugawanywa.
Licha ya changamoto inayo msubiri Malcolm Turnbull amesisitiza kuwa mfumo waku gawa mapato ya GST, unastahili kuwa sawa kwa wa Australia wote.
Hata hivyo serikali kadha za mikoa nchini zime apa kuto badili mfumo wa mapato ya GST, bila kuafikiana na serikali zingine za mikoa na majimbo hali ambayo huenda ika sababisha pendekezo la Bw Turnbull kufeli.
Share





