Aina hiyo ya muziki ambao uli fanywa maarufu duniani kote na wasananii kama Bob Marley, ume tambuliwa kwa mchango wake katika maswala ya haki ya jamii, maendeleo ya tamaduni mbali mbali, pamoja na uvutio wake duniani kote.
Baadhi ya tamaduni zingine zisizo onekana ambazo ziliongezwa katika orodha ya umoja wa mataifa, ni kama uundaji wa bobbin lace kutoka Slovenia, miereka ya Chidaoba kutoka Georgia, mchezo wa hurling kutoka Ireland, maonesho ya asili yakuzaliwa kwa Yesu kwa jina la szopka kutoka Poland, pamoja na wafugaji wa farasi wa jadi kutoka Kazakhstan.