Mabadiliko ya tabianchi yanapo sababisha ongezeko ya hali ya joto na mazingira ya ukame, tunaweza tarajia moto ya vichaka mikali zaidi mara kwa mara katika siku za usoni.
Wa Australia hukumbushwa mara kwa kara kuhusu umuhimu wakuwa na mpango wa moto wa vichaka.
Ila, nini hutokea wakati miali ya moto kutoweka? Moto unapo zimwa, unarudije nyumbani salama, unapataje msaada naku jihudumia?
Kuanzia kwa majibu ya dharura, hadi uponaji wa muda mrefu, sikiza maelezo ya wataalam waki elezea hatua muhimu zakuchukua baada ya moto wa vichaka. Kupona kutoka kwa moto wa vichaka ni safari ndefu ila, si lazima ukabili hali hiyo ukiwa mwenyewe.
Kuna msaada kwa usalama wako, nyumba yako na ustawi wako.
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Yafafanuliwa, kwa taarifa na vidokezo muhimu zaidi kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Je una swali au pendekezo ya mada? Tutumie barua pepe kwa anwani hii australiaexplained@sbs.com.au




