Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amezindua Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya vyama vya CCM na ACT-Wazalendo, uteuzi huo wa wajumbe 10 unaashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Hatua hii inakuja baada ya vyama vya CCM na ACT Wazalendo kusaini Tamko la Pamoja la Makubaliano ya Julai 9 mwaka huu, hivyo jukumu kubwa sasa ni kugeuza makubaliano hayo ya kisiasa kuwa hatua zinazotekelezeka.
Wakati Kenya ikielekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, jina la Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, linaendelea kujitokeza kama mojawapo ya viongozi wanaowavutia wananchi, hasa vijana. Licha ya umaarufu wake kuongezeka, Sifuna bado hajatangaza rasmi nia ya kuwania urais. Hata hivyo, mikutano yake imekuwa ikiwavutia maelfu ya watu licha ya kuwepo kwa mazingira ya vitisho na vurugu za kisiasa dhidi ya wapinzani. Sifuna amesema kuwa vijana wanapaswa kuaminiwa kuingoza Kenya.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






