Hatimae seneti ime pitisha muswada wa serikali wa mashirika ambayo yamesajiliwa, baada yakushiriki katika mjadala uliofikia tamati yake alfajiri ya leo mjini Canberra.
Muswada huo ulikuwa moja ya maswala mawili yaliyo tumiwa na serikali kuvunja bunge mnamo mwezi julai nakuitisha uchaguzi mkuu nchini.
Swala la pili laku anzisha tume inayo chunguza sekta ya majengo na ujenzi, bado lina jadiliwa kati ya serikali na wabunge kutoka vyama vidogo na baadhi yawa bunge huru.
Kura kwa muswada huo ilijiri baada ya kura nyingine ndani ya seneti usiku wa jana jumatatu ambako, baadhi yama seneta wa chama cha Nationals, kupiga kura dhidi ya serikali kuhusu pendekezo lakupiga marufuku kuingizwa nchini kwa bunduki aina ya Adler.
Share





