Taarifa hiyo imejiri wakati Australia imeripoti siku nyingine, yakutokuwa na visa vyovyote vya maambukizi katika jamii.
Na jimboni Victoria, hapakuwa kesi zozote mpya kwa siku ya tatu mfululizo ila, mamlaka huko wame kiri kuwa huenda hawataweza baini jinsi mfanyakazi katika hoteli ya karantini alivyo ambukizwa virusi hivyo. Mamlaka husika wanafanya tathmini ya vifaa vyakusambaza hewa ndani ya hoteli zote za karantini jimboni Victoria, pamoja na kinga za sura ambazo nilazima zivaliwe na wafanyakazi.
Kwa hatua za afya na msaada ambazo zimewekwa, katika jibu la janga la COVID-19 katika lugha yako, tembelea tovuti hii: sbs.com.au/coronavirus