Janga la coronavirus limesababisha uharibifu mkubwa katika nchi nyingi na maisha ya watu binafsi duniani kote.
Viongozi wa jamii mbali mbali nchini Australia wameweka mikakati yakuwanusuru, wanachama wa jamii zao dhidi ya janga la coronavirus ambalo linaendelea kusababisha uharibifu mkubwa duniani kote.
Shirika la Kenya Community Victoria, linajiandaa kutoa misaada mbalimbali kwa wakenya wanao ishi jimboni Victoria watakao athirika na COVID-19.
Mweka hazina wa shirika hilo Jason Njuguna, alieleza idhaa ya Kiswahili ya SBS kuhusu baadhi ya hatua ambazo shirika lake lime andaa kuwasaidia wakenya wenzao.
Share






