Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohamed Salah wamechaguliwa kwa tuzo ya Mchezaji bora wa FIFA.
Lakini hakuna nafasi kwa ajili ya Barcelona na nyota wa Argentina Lionel Messi.
Mchambuzi wa soka wa Afrika Mashariki George Ambangile ambaye anafanya kazi Magic FM huko Dar es Salaam - Tanzania, alielezea habari hiyo ya kushangaza kama alivyohojiwa na Mtayarishaji wetu wa SBS, Frank Mtao.






