Taarifa ya Habari 1 Februari 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Waziri Mkuu amekiri kuwa wapiga kura wamekerwa baada ya msimu wa majira ya joto, ulio tawaliwa na usambaaji wa wimbi la virusi vya Omicron vya UVIKO-19, ongezeko ya vifo vya coronavirus pamoja na uhaba wa vipimo vya rapid antigen.


Maeneo ya kanda ya jimbo la Kusini Australia yame gongwa na dhoruba na mafuriko ya ghafla, hali ambayo imesababisha kufungwa kwa barabara kuu nyingi, pamoja na wito wa misaada kwa huduma za dharura. Eneo la APY jimboni humo limepata pigo kubwa zaidi, eneo hilo lilipata mili lita 160 ya mvua usiku wakuamkia, ambayo ni takriban nusu ya kiwango cha mvua ambayo hunyesha mjini humo kila mwaka.

Kuna harakati ndogo kwenye mpaka wa Gatuna kati ya Rwanda na Uganda ambao umefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa takriban miaka mitatu. Mpaka huo ulifungwa mwaka 2019 kufuatia mivutano baina ya mataifa hayo ya Afrika mashariki. Kwa upande wa Uganda, ujenzi wa ofisi za forodha ambazo ni sehemu ya mfumo wa kituo kimoja cha mpakani unaotekelezwa katika jumuiya ya Afrika mashariki unaendelea.

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Jumatatu umetangaza kwamba umerejesha hali ya kutekeleza katiba ya nchi wiki moja baada ya kuchukuwa madaraka na kumteua kiongozi wa mapinduzi hayo kuwa mkuu wa nchi kwa kipindi cha mpito. Hatua hiyo imejiri muda mfupi baada ya Umoja wa Afrika kusitisha uanachama wa Burkina Faso kutokana na mapinduzi ya kijeshi Jumatatu iliyopita, huku wanadiplomasia kutoka Afrika magharibi na Umoja wa Mataifa wakishinikiza kurejea kwa utawala wa kiraia.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service