Taarifa ya habari 1 Novemba 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Historia yatengezwa katika uchaguzi wa Queensland na serikali ya shirikisho, yazindua kampeni yakusaidia jamii kukabiliana na changamoto za afya ya akili.


Waziri katika baraza la mawaziri la Uingereza Michael Gove amesema muda wa mwezi mmoja wa kufunga kabisa shughuli za kichumi za taifa hilo katika kukabiliana na virusi vya corona unaweza kuongezwa.

Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli hatimaye amepokea cheti cha ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliokamilika. Wakati huo huo vyama vikuu viwili vya upinzani nchini Tanzania, vimetaka kurejewa kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na vilevile kutoa wito kwa Watanzania kufanya maandamano yasiyo na kikomo, kuanzia Jumatatu hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ameonya kwamba taifa hilo la Afrika magharibi linaweza kuingia kwenye machafuko makubwa iwapo wagombea kwenye uchaguzi wa jumamosi, hawatosuluhisha mvutano uliosababisha maandamano ya vurugu na wito wa upinzani wa kususia uchaguzi.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service