Taarifa ya habari 10 Januari 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Wakazi wa eneo pana la Brisbane kupata afueni baada ya vizuizi kuregezwa, na wakazi wa maeneo ya milipuko ya COVID-19 jimboni NSW waombwa kuendelea kufanya tahadhari.


Wabunge wa Democrats wanapanga kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Donald Trump kwa mchango wake katika vurugu za uvamizi wa bunge zilizotokea Jumatano katika bunge la Marekani. Msemaji wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema atawasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Bwana Trump ikiwa hatajiuzulu mara moja.

Waziri wa Usafiri wa Indonesia anasema Shirika la Ndege la Sriwijaya limepoteza mawasiliano na moja ya ndege zake za abiria mara baada ya kuruka kutoka Jakarta Jumamosi. Ndege SJ182 ilikuwa inaelekea Pontianak katika kisiwa cha Borneo. Zaidi ya watu 50 walikuwa wakisafiri katika ndege hiyo, maafisa wamesema.

Wakuu wa usalama nchini Uganda wameonya wapiga kura nchini humo kutosalia katika kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura yao. Uganda inafanya uchaguzi mkuu alhamisi wiki ijayo. Kampeni za uchaguzi zimeshudia machafuko, vifo na kukamatwa kwa wafuasi na wagombea wa upinzani.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service