Chama cha Labor kime kiri itakuwa vigumu sana kushinda eneo bunge hilo la Qld, kwa sababu utabiri wote unao onesha mgombea wa chama cha Liberal Cameron Caldwell, anatarajiwa kuibuka mshindi.
Chaguzi hilo dogo lili sababishwa na kujiuzulu kwa Waziri wa zamani Stuart Robert, ambaye alishinda eneo bunge hilo latika uchaguzi wa 2022 kwa 10.6% ya kura.
Mgombea wa chama cha Labor Letitia Del Fabbro, amesema anafurahia kuwania eneo bunge hilo tena, hataka kama ni eneo salama la Liberal. Chama cha Labor kime wahi shinda eneo bunge la Fadden mara moja tu, katika uchaguzi wa 1983 chini ya ya serikali ya Hawke.
New South Wales itatuma kundi la nne la wazima moto Canada, wakati zaidi ya visa 800 vya moto vina endelea kukabiliwa kote nchini humo.
Zaidi ya wazima moto 50 pamoja na mashirika ya huduma ya dharura, yana elekea Canada, hatua ambayo imefikisha idadi ya watu ambao wame tumwa huko mwaka huu kupita 700.
Canada imukuwa na zaidi ya mioto 3,900 ambayo imechoma zaidi ya hekta milioni 9.7, ambayo ni takriban mara mbili ya sehemu iliyo chomeka jimboni NSW wakati wa tukio la moto wa vichaka la majira ya joto.
Mwanaume mmoja kutoka Darwin amekubali ana hatia kwa mashtaka zaidi ya 30, baada yaku kamatwa akiwa na zaidi ya video 500 pamoja na picha 300 zinazo onesha matendo ya unyanyasaji wa binti yake wakambo.
Mwanaume huyo amekubali mashtaka 31 yanao jumuisha kutumia mtoto kwa utengenezaji wa nyezo za unyanyasaji wa watoto na kwa kutumia mtoto mwenye chini ya miaka 16 kwa njia isiyofayaa.
Mahakama ya juu alielezwa mwanaume huyuo alikuwa sehemu ya vikundi kadhaa vinavyo jadili mada kama watoto wachanga wakike pamoja na matendo ya ukatili dhidi ya wanyama.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC Karim Khan, amesema kwamba ofisi yake inchunguza ripoti kwamba miili ya watu 87 ilipatikana katika kaburi la pamoja katika jimbo la Dafur, maghaaribi mwa Sudan.
Karim Khan ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mahakama ya ICC ina mamlaka ya kuchunguza uhalifu uliofanywa Darfur na kwamba inachunguza vurugu zilizotokea huko tangu mapigano yalipoanza April 15 kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi la dharura RSF.
Kumekuwepo na ripoti kadhaa za vurugu dhidi ya raia hasa katika mji wa El Geneina, huko Darfur Magharibi.
Chama cha upinzani cha Ensemble pour la République kinachoongozwa na Moise Katumbi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimetaka ufanyike uchunguzi huru baada ya kuuawa mbunge wake, Chérubin Okende siku ya Alhamisi
Cherubin Okende alikuwa mwanachama wa chama cha Moise Katumbi, kiongozi maarufu wa upinzani ambaye anatazamiwa kuwania uchaguzi wa rais katika taifa hilo la Afrika ya Kati hapo Desemba.
Baada ya kupatikana mwili wake serikali iliiagiza haraka mahakama kuanzisha uchunguzi ili kubaini ukweli zaidi kuhusu mauaji hayo. Mshukiwa wa kwanza akiwa ni mlinzi wake tayari amekamatwa kwa uchunguzi na sasa yupo korokoroni akihojiwa.
Waziri wa ujenzi na uchukuzi wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa ametetea hatua ya serikali kuingia makubaliano ya ushirkiano na kampuni ya DP World akitaja uwezo mkubwa wa kampuni hiyo kuwezesha bandari kote duniani.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa ametaja sababu za serikali kuanzisha majadiliano na kampuni ya DP World, kuwa ni pamoja na uwezo wake mkubwa katika uwezeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia Ulaya, Amerika ya Kaskazini, lakini pia ile ya kusini na Australia. Hii na mara ya kwanza kwa serikali kujitokeza kwa wahariri wakati sakata la mkataba huo likiendelea kuwa mada moto inayojadiliwa kila uchao.
Na katika taarifa za michezo, Australia ime shinda mechi yake yakirafiki dhidi ya Ufaransa kwa goli moja kwa 0 katika sehemu ya maandalizi ya kombe la dunia la mpira wa miguu wa wanawake, na katika michuano ya raga Wallabies kumenyana na Pumas wa Argentina mjini Parramataa, NSW leo jioni.