Taarifa ya Habari 2 Septemba 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Mbunge wa upinzani Matt Canavan amesema sera za uhamiaji za seriakli, zina wasukumu watu kuwa na maoni yenye misimamo mikali. Amesema serikali ya Labor imefungua anacho ita milango ya mafuriko ya uhamiaji baada ya janga la UVIKO-19, na inawaruhusu watu kuingia nchini kiholela chini ya ya sera zake za sasa.


Naibu kiongozi wa jimbo la Victoria ambaye pia ni waziri wa Elimu jimboni humo, Ben Carroll, ametangaza hatua yakupanua mradi wa vilabu vya viamsha kinywa vya shule, mradi mhimu waku hakikisha wanafunzi wana anza siku ya shule wakiwa na lishe na tayari kujifunza. Kupitia jeki ya hivi karibuni ya uwekezaji wa milioni A$21.1 katika bajeti ya 2024–25, mradi huo sasa unatolewa kwa kila shule ya serikali jimboni Victoria, shule 150 za ziada zikijiunga na imekadiriwa kuwa idadi ya wanafunzi laki sita wana faidi kupitia mradi huo.

Nchini Uganda, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, Kizza Besigye, hakuhudhuria ufunguzi wa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatatu asubuhi Septemba 1, katika Mahakama Kuu ya Kampala. Akiwa amezuiliwa tangu kukamatwa kwake nchini Kenya mwezi Novemba mwaka jana, mmoja wa mawakili wake amedai kuwa mteja wake alikuwa akisusia kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mtanange wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, nchini Tanzania umeingia katika hatua mpya baada ya vyama vya siasa kuzindua kampeni zao. Ahadi zinazotolewa na wagombea wa urais wa vyama 17 vinavyoshiriki uchaguzi huo zimeibua maswali. Vita ya kisiasa sasa rasmi vimehamia majukwaani, vyama vikijaribu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika oktoba 29.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service