Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt amesema vikao vya bunge la shirikisho vitakapo anza tena, chama chake kita pendekeza muswada waku hakikisha wafanyakazi wote wana weza pata malipo ya siku 14, kujitunzisha coronavirus.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu aliyepigwa risasi mara kumi na sita katika shambulizi la mwaka 2017 amerudi nchini humo kutoka uhamishoni ili kukabiliana na Rais John Pombe Magufuli katika kinyang'anyiro cha kuwania urais.
Serikali kadhaa duniani zimechukua hatua za kurejesha vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya corona zikijaribu kuepuka wimbi jipya la maambukizi wakati idadi ya vifo vilivyotokana na COVID-19 imepindukia 650,000.