Taarifa ya habari 4 Agosti 2020

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Serikali ya Victoria imewasilisha adhabu kali zaidi, kwa watu wanao feli kubaki ndani ya karantini, faini za $5000 za papo hapo zitatolewa kwa watakao kiuka amri husika.


Mamlaka ya kupambana na ufisadi nchini Afrika kusini ilisema Jumatu ilisema inachunguza madai ya ufisadi katika utoaji wa zabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kupambana na janga la Corona nchini humo.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimempitisha Makamu Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kuwania urais na hivyo kufunguwa njia kwa mahasimu wawili wakubwa nchini humo kuchuwana kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28. Dkt John Pombe Magufuli atawakilisha chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu.

Wanaanga wawili wa Marekani Doug Hurley na Bob Behnken wako katika safari ya mwisho na sehemu muhimu ya majaribio ya chombo cha kampuni binafsi cha SpaceX kurejea duniani, Jumapili.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya habari 4 Agosti 2020 | SBS Swahili