Jibu la serikali ya Wilaya ya Kaskazini kwa uhalifu wa vijana, limejadiliwa katika tamasha ya Garma ya mwaka huu. Viongozi wa jamii walizungumza kuhusu mfumo wa kizuizi wa vijana katika wilaya ya Kaskazini na, wameiomba serikali ya shirikisho iingilie kati na isitishe hatua za haki ambazo zime undwa kukabiliana na uhalifu wa vijana.
Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi anaripotiwa kuwa anakaribia kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri. Jumamosi, Agosti 2, alithibitisha nia yake kwa viongozi wa Muungano Mtakatifu, jukwaa lake la kisiasa. Tangazo lingine: serikali itapunguzwa. Itapunguzwa hadi chini ya wajumbe 50, ikilinganishwa na 54 wa sasa.
Miaka mitano ya uhai wa bunge la 12 la Tanzania, ulitamatika Jumapili ya wikendi iliopita kufuatia tangazo la rais Samia Suluhu Hassan, kulivunja bunge hilo kwa mujibu wa katiba.
Kuvunjwa kwa bunge hilo kunafungua ukurasa mwingine kwa vyama vya siasa kuanza kuteua wagombea wa nafasi za ubunge kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.