Baraza la Huduma ya Jamii ya Australia, limesema juhudi za serikali ya shirikisho kutoza hela kwa maombi ya uhuru wa taarifa, kunaweza rejesha aina ya unyanyasaji wa mfumo wa malipo ya deni ya robodebt muswada huo ukipitishwa.
Wanaharakati wa haki za binadam wameikosoa serikali ya shirikisho kwa kuharakisha sheria mpya za kuwafurusha watu nchini, kupita bungeni jana. Mswada huo ni sehemu ya juhudi ya serikali kutatua, tatizo lakisheria la kundi la NZYQ ambao ni takriban raia 280 ambao si raia, walio achiwa kutoka kizuizi cha muda mrefu cha uhamiaji kwa sababu ya uamuzi wa mahakama kuu katika mwaka wa 2023.
Ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ule wa waasi wa AFC/M23, umekuwa jijini Doha kwa wiki tatu sasa kwa ajili ya mazungumzo ya amani, lakini hatua kubwa haijapigwa. Ripoti kutoka kwenye mazungumzo hayo, zinasema, mpaka sasa hakuna mazungumzo muhimu yaliyofanyika.
Ukiwa na zaidi ya hekta 1,000, Msitu wa Karura ni msitu wa pili kwa ukubwa wa mijini ulimwenguni. Tangu mwaka wa 2009, kutokana na kujitolea kwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Wangari Maathai, hifadhi hii ya asili imekuwa ikisimamiwa kwa pamoja na wakazi jirani ya msitu huu, wanaojumuika katika Chama cha Friends of Karura, na serikali.