Mji wa Nagasaki nchini Japan leo umefanya kumbukumbu ya miaka 75 tangu uliposhambuliwa kwa bomu la nyuklia na Marekani ambapo meya na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wameonya juu ya matumizi ya silaha za nyuklia.
Watu wasiopungua tisa wameuawa na takriban wengine 20 kujeruhiwa Jumamosi katika mlipuko wa bomu lililokuwa ndani ya gari mbele ya mlango wa kuingilia kwenye kituo cha kijeshi mjini Mogadishu, mashahidi na maafisa wa usalama wamesema.
Shirika la ndege la Kenya Airways linasema kuwa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania haijabatilisha uamuzi wa kufuta kibali cha kuziruhusu ndege zake kusafiri nchini humo takriban wiki moja baada ya Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia kueleza kuwa nchi hizo mbili zimefikia makubaliano.