Serikali ya Ghana imetangaza kuwa itawarudisha raia wake 300-wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia ongezeko la visa vya wageni kushambuliwa.
Waziri wa Mambo ya nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema rais John Dramani Mahama, ameidhinisha hatua hiyo. Hatua hii inakuja, baada ya raia wa Ghana wanaoshi nchini Afrika Kusini, kuomba kurejea nyumbani baada ya kuripoti matukio ya kushambuliwa na biashara zao kuvamiwa na kuharibiwa kwa madai kuwa, wageni wamekuja kuchukua ajira wenyeji.
Kiongozi wa Upinzani, Angus Taylor, atatumia hotuba yake ya kwanza ya kujibu bajeti kuhusisha idadi ya wahamiaji wanaoingia Australia na idadi ya nyumba mpya zinazojengwa. Hotuba hiyo itaainisha mpango wa kudhibiti uhamiaji na kuweka ukomo wa idadi ya watu wanaohamia nchini, kulingana na idadi ya nyumba zilizojengwa mwaka uliopita.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.






