Mahakama Kuu ya Kenya Jumanne ilisimamisha kwa wiki tatu zaidi mpango wa kujenga kituo cha karantini ya Ebola, kilichopendekezwa na Marekani.
Jaji wa mahakama hiyo Patricia Nyaundi, ametoa amri inayoikataza serikali ya Kenya kuchukua hatua yoyote ya kujenga au kuanza shughuli katika kituo hicho kilichopangwa kujengwa mjini Nanyuki hadi kesi hiyo itakapomalizika.
Serikali ya shirikisho itajaribu kupitisha sehemu ya kwanza ya hatua zake za bajeti zilizopendekezwa kupitia bunge la chini leo [[04/06]], wakati kukiwa na upinzani mpya kuhusu mabadiliko ya kodi. Sehemu ya kwanza inatarajiwa kuharakishwa kupitia bunge la chini.
Kocha mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anasema kuna chaguzi kadhaa ambazo zipo tayari kwa ajili yao kucheza, kufuatia usumbufu kutokana na mlipuko wa Ebola unaowakabili kabla ya Kombe la Dunia. Timu hiyo tayari imelazimika kughairi mchezo wakirafiki dhidi ya Chile wiki ijayo, baada ya meya wa jiji huko Uhispania ambapo mchezo huo ungechezwa kusaini amri ya kuzuia mechi hiyo.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






