SKIP TO MAIN CONTENT

Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji inayo imarisha sheria kwa wanafunzi wakimataifa na watalii

TONY BURKE PRESS CLUB
Australian Home Affairs Minister Tony Burke speaks at the National Press Club of Australia in Canberra, Thursday, October 16, 2025. (AAP Image/Lukas Coch) NO ARCHIVING Source: AAP / LUKAS COCH/AAPIMAGE

Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji, ambayo inaimarisha sheria kwa wanafunzi wa kimataifa na watu ambao wako nchini kwa likizo, inalenga wanao baki nchini zaidi ya muda wa viza zao na wanaohama kutoka viza moja hadi nyingine, na inawapa kipaumbele wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta muhimu.


Published

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS


Skip to podcast episode content

Serikali ya shirikisho inatetea hatua yake kali ya uhamiaji, ambayo inaimarisha sheria kwa wanafunzi wa kimataifa na watu ambao wako nchini kwa likizo, inalenga wanao baki nchini zaidi ya muda wa viza zao na wanaohama kutoka viza moja hadi nyingine, na inawapa kipaumbele wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta muhimu.


Jimbo la Queensland limekataa kufuata mwongozo wa serikali ya New South Wales katika kuwaruhusu madereva wenye kiasi kidogo cha bangi katika mfumo wao kuwa barabarani. Sheria ya kuondoa marufuku kwa wagonjwa wanao tumia bangi kama dawa imepitishwa ndani ya bunge la New South Wales, ikiwaruhusu madereva wenye leseni isiyo na vikwazo kuendesha gari mradi tu wamesajiliwa kama watumiaji wa dawa waliosajiliwa na wana uthibitisho wa agizo halali la daktari.

Watu watano, wakiwemo maafisa wawili wa Kitengo cha Kupambana na Wizi wa Mifugo (ASTU), wameuawa katika shambulio la watu wenye silaha katika eneo la Gotu, Kaunti ya Isiolo nchini Kenya. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Isiolo, Isaac Sang, maafisa hao walikuwa sehemu ya kikosi kilichokuwa kikifuatilia washukiwa wa wizi wa mifugo walipovamiwa na washambuliaji wenye silaha mapema Jumatano.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now