Serikali ya shirikisho ime tangaza mabadiliko makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Australia, ikiimarisha sheria kuhusu ni nani anayeweza kuja nchini na ni nani anayeweza baki nchini.
Marekebisho hayo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu yatawazuia wanafunzi wa kimataifa kuwaleta wanafamilia Australia, kuwazuia watu kutumia visa ya wageni ili kuongeza muda wao wa kubaki nchini, kuimarisha sheria za kuhama kutoka visa moja hadi nyingine, na kuimarisha juhudi za kuwaondoa watu ambao hawana visa halali tena. Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke anasema moja ya mabadiliko makubwa zaidi yatakomesha uwezo wa wanafunzi wa kimataifa kuwajumuisha kiotomatiki wanafamilia kwenye visa za wanafunzi na wahitimu.
Serikali ya Kenya itakata rufaa dhidi ya uamuzi uliobatilisha mauzo ya hisa za Safaricom kwa dola bilioni 1.9. Wachambuzi wanaonya kuwa hatua hiyo inaweza kuhatarisha mpango mkubwa wa miundombinu wa Rais William Ruto. Mahakama imesema uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za serikali kwa kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini ulikiuka masharti kadhaa ya kisheria na kikatiba. Serikali imesisitiza kuwa taratibu zote zilifuatwa.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






