Watatu hao ni sehemu ya kundi la zaidi ya wanawake na watoto kumi na wawili waliowasili Sydney na Melbourne jana usiku (Alhamisi). Familia hizo zililakiwa uwanja wa ndege na polisi, wafuasi, na vyombo vya habari.
Serikali ya Shirikisho imefichua mipango mipya ya kuwalazimisha wauzaji nje wa gesi kuelekeza asilimia 20 ya bidhaa zao kwenye soko la nishati ya ndani. Katika juhudi za kupunguza bei na kuepuka uhaba wa muda mrefu, Waziri wa Nishati Chris Bowen anasema akiba ya gesi ya pwani ya mashariki itaona moja ya tano ya mauzo ya nje ikitengwa kwa ajili ya matumizi nchini Australia kuanzia katikati ya 2027.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amedokeza juu ya uwezekano wa kuwania muhula wa tatu, na kuchelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa katika muda wa miaka miwili ijayo. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Jumatano mjini Kinshasa, Tshisekedi alisema hajaelezea nia ya kutaka muhula wa tatu, na kuongeza lakini kuwa ikiwa watu watamtaka kuendelea, atakubali.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





