Zaidi ya idadi yawa Australia takriban 2000, ambao wanakabiliana na visa sugu vya melanoma, hivi karibuni wata pokea msaada wakifedha, baada ya mfumo wa matibabu kupanuliwa katika mfumo wa mafao ya madawa almaarufu PBS. Kuanzia leo tarehe mosi Machi, dawa kwa jina la Opdivo (nivolumab) ambayo imeorodheshwa katika mfumo wa PBS, itapanuliwa nakuwasaidia wagonjwa 1500, ambao bila msaada huo wangepashwa lipa zaidia ya $100,000 kwa kila tiba bila msaada huo wa PBS.
Marekani na kikundi cha Taliban wamesaini makubaliano Jumamosi mjini Doha, Qatar, wakiandaa mazingira kumaliza vita vilivyodumu kwa takriban miaka 19 nchini Afghanistan na hivyo Marekani kurejesha vikosi vyake vilivyoko nchini huko.
Chama tawala nchini Tanzania CCM kimemfukuza uanachama aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bernard Membe.
Membe alikuwa akikabiliwa na tuhuma za maadili pamoja na viongozi wengine waandamizi wengine wawili makatibu wakuu wa zamani Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, ambao wao hawajafukuzwa. Makamba amesamehewa, huku Kinana akionywa kwa karipio.
Washambuliaji wamewaua watu 24 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Gavana wa mkoa wa Ituri ulioko kaskazini mashariki mwa Congo. Gavana Jean Bamanisa amesema washambuliaji wametumia mapanga na bunduki kuwaua raia ambapo askari waliitwa kurejesha hali ya usalama kufuatia shambulio hilo.