Mweka hazina wa taifa John Frydenberg amekadiria kuwa dharura yakimataifa ya coronavirus, itakuwa na athari kubwa zaidi kwa uchumi wa australia, ikilinganishwa na moto wa vichaka wa msimu huu wa majira ya joto.
Serikali ya Ujerumani imeahidi kufadhili miradi ya elimu, na kupiga jeki uzalishaji katika viwanda nchini Kenya ili kukabiliana na tatizo ya ajira ambalo linazidi kuongezeka nchini Kenya.
Watu 12 wenye silaha wameripotiwa kuuawa katika mapigano na vikosi vya kulinda usalama vya serikali ya Burundi, yaliotokea jumapili katika wilaya moja kusini mwa mji mkuu Bujumbura.