Wa Australia walio kuwa wame kwama nchini China, wakati mlipuko wa coronavirus ulipo tangazwa, wame elezea shukrani zao kwakurejeshwa nyumbani.
Vikosi vya usalama nchini Ujerumani vinajiandaa kwa uwezekano, wa kutokea mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia tukio la wiki hii la ufyatuaji risasi, katika mji wa magharibi mwa Ujerumani Hanau
Mamia ya wananchi wa Rwanda wamejitokeza Jumamosi, kuuaga mwili wa msanii maarufu wa nyimbo za Injili Kizito Mihigo, akiwemo Diane Rwigara, mwanasiasa wa upinzani na mfanyabiashara mjini Kigali.
Rais wa Sudan Kusini amechukua hatua ya kihistoria iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu, kwa kulivunja baraza la mawaziri na kumchagua kiongozi wa upinzani Riek Machar, kuwa makamu wa kwanza wa rais, siku moja kabla ya kuapishwa Jumamosi kwa serikali ya mpito ya umoja wa taifa.