Taarifa za habari: Mamlaka wa Australia, wakabiliwa kwa ongezeko la ombi la vipimo vya Coronavirus

Patients line up at the Royal Melbourne Hospital for Coronavirus testing.

Patients line up at the Royal Melbourne Hospital for Coronavirus testing. Source: AAP

Afisa mkuu wa afya wa australia, Brendan Murphy, asema mamlaka wamekabiliwa kwa maombi mengi, yakufanyiwa vipimo baada yakuonesha dalili kama za mafua.


Huduma yakisheria ya Victoria imeomba mageuzi ya mchakato wakubadili jina, kwa wahanga wa vurugu ya nyumbani kupitia mashirika yaku idhinisha irahisishwe.

Waathiriwa wa vurugu ya nyumbani wanaweza omba mahakama kubadili majina yao ila, kama waliolewa ng'ambo, watu wa Victoria wanaweza wasilisha maombi yao kupitia sajili yakuzaliwa, vifo na ndoa. Mahakama ya shirikisho imesema ina rasilimali zakuwasaidia wahamiaji, wakati idara ya haki ya Victoria imesema kwamba, sajili yakuzaliwa, vifo na ndoa ina nafasi yakuomba msaada unapo kabiliwa kwa matatizo yakifedha.

Afghanistan imetumbukia zaidi katika mzozo wa kisiasa Jumatatu baada ya viongozi wawili hasimu - Rais Ashraf Ghani na Abdullah Abdullah kujipaisha kuwa marais katika hafla mbili sawia zilizovurugwa na milipuko ya mabomu.

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amerejea ofisini leo mchana, saa chache baada ya jaribio la kumuua kushindwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum. Msemaji wa baraza la mawaziri, Faisal Mohamed Salih amesema kiongozi huyo anaendelea na majukumu yake ofisini kama kawaida.

Maafisa wa wizara ya afya nchini Uganda siku ya Jumapili wamesema kwamba takriban raia 22 wa kigeni watarudi katika mataifa yao huku hofu ya maambukizi ya virusi vya corona ikiendelea.Kulingana na waziri ya afya nchini humo raia hao walikataa kwenda karantini kwa siku 14 walipowasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe.

 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service