Masaibu yakuwa mtoto wa barabarani Burundi
Getty images Source: Getty Images
Burundi kama mataifa mengine ya bara la Afrika inakumbwa na changamoto ya kuwepo kwa watoto wanaorandaranda barabara mijini. Taifa hilo linalopitia vipindi vya machafuko na vita, limekuwa linashuhudia ongezeko la watoto wa barabarani kila uchao. Maisha duni ndani ya familia pia ni sababu inayoelezewa kusababisha idadi ya watoto hao kuongezeka. Mji mkuu wa Bujumbura, unakisiwa kuwa na watoto wa barabarani zaidi ya elfu mbili kwa jumla ya watoto wanaokadiriwa kuwa 3500 katika nchi nzima. Serikali ya nchi hiyo imeandaa sera ya kuwaondoa watoto hao barabarani, lakini uwezo wa kufadhili mpango huo ndio changamoto. Kutaka kujua upana wa tatizo hilo, mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani Kibuga, ametuandalia taarifa ifuatayo. Ungana naye.
Share




