Key Points
- Cervical screenings save lives by detecting the presence of the human papillomavirus.
- If not detected early, HPV infections can lead to serious health problems including cancer.
- Women from multicultural backgrounds are under-screened.
- Self-screening removes cultural barriers to testing.
Zaidi ya asilimia 70 ya kesi za saratani ya kizazi hutokea kwa watu ambao hawaja wahi fanya vipimo, au ambao muda wakufanya vipimo umepita?
Hiyo ni sababu nzuri yakupimwa, au kinacho itwa uchunguzi wa kizazi.
Uchunguzi wa kizazi husaidiaje kuzuia saratani ya kizazi?
“Hufanya hivi kwa kwa kutambua mapema mabadiliko katika seli za kizazi, haswa uwepo wa papillomavirus ya binadamu, ambayo inaweza sababisha mabadiliko ya seli ambayo inaweza geuka kuwa saratani baada ya muda,” Dr Ahlam Ibrahim amesema. Yeye ni GP mjini Sydney, mwalimu wa jamii na mwanzilishi wa shirika la Sudanese Australian Health Wellbeing Association.
Kutambua mapema mabadilio ya seli, kuna maana zinaweza fuatiliwa naku tibiwa kabla iwe saratani.
Uchunguzi wa saratani ya kizazi husimamiwa na Mradi wa Kitaifa wa Uchunguzi wa Saratani ya Kizazi maarufu kwa kifupi NCSP. Lengo la NCSP nikutambua kila mtu ambaye yuko katika hatari yakupata papillomavirus ya binadam, inayo julikana pia kwa ufupi kama HPV. Na unapo fanya uchunguzi wako wa kwanza, wata kutumia kumbusho wakati uchunguzi mwingine utakuwa.

When it comes to cervical screening, women from multicultural backgrounds are being left behind, and particularly newly arrived women.
Nani anastahili fanya uchunguzi wa kizazi?
Jibu ni mtu yeyote ambaye yuko katika hatari yakuwa na HPV.
Uchunguzi huo unapendekezwa kwa wanawake wote na watu wenye kizazi chenye umri kati ya miaka 25 na 74 na pia kwa ambao wame wahi kujamiana. Dr Ibrahim amesema.
“Uchunguzi huo hufanywa kila miaka mitano, ilimradi matokeo niya kawaida. Hata kama umepaa chanjo ya HPV kabla, bado unastahili fanyiwa uchunguzi mara kwa mara kwa kirusi hicho kwa sababu, chanjo hiyo haifuniki aina zote za saratani zinazo sababisha HPV.”
Nawezaje fanyiwa uchunguzi?
Unaweza tembelea GP wako, zahanati ya afya ya jamii au zahanati ya afya ya wanawake na baadhi ya huduma za Matibabu zawa Aboriginal.
Kama una kadi ya Medicare kawaida malipo ya miadi yako hugharamiwa kwa mfumo wa bulk billing ambako serikali huchangia kufunika gharama ya huduma, kwa hiyo hauta kuwa na gharama yoyote.
Hata hivyo, unaweza pata gharama ukimtembelea daktari ambayo hatoa huduma ya bulk billing.
Kuna aina mbili za uchunguzi zinazo tolewa. Wakati wa miadi yako, mtoaji wako wa huduma ya afya ata kuelezea kuhusu chaguzi hizo mbili.
Aina hizo mbili za chunguzi ni gani?
Unaweza amua daktari wako au muuguzi akufanyie uchunguzi huo ndani ya zahanati.
“Tuna chukua sampuli kwa kutumia brashi ndogo kutoka sehemu ya juu ya kizazi,” Dr Ahlam ame elezea.
Sasa kuna chaguzi yaku jichukulia sampuli mwenyewe, bila msaada wa mtaalam wa afya.
“Hii inaruhusu mtu achukue sampuli kwa kutumia kifaa kidogo ambacho kinaweza ingizwa ndani ya kizazi. Ni faragha, chaguzi rahisi na pia ni sahihi kwa kutambuliwa kwa HVP.”
Kila uchunguzi unastahili chukua dakika chache tu.

Dr Ahlam Ibrahim
Faida ni gani za kujikusanyia sampuli?
Mtumiaji wa Afya Jyotsna Oliver alihudhuria kikao cha habari ya jamii ambako, alijifunza kuhusu chaguzi ya kujikusanyia sampuli.
“Kama sote tunavyo jua kuhusu uchunguzi wa kizazi, daima tume ihusisha na maumivu kidogo, kimwili na kihisia kwa sababu mara nyingi kuna hisia ya kuathirika wakati wa miadi hiyo inayo ongozwa na daktari.” Bi Oliver amesema.
“Na ndiyo sababu, nilipo jua kuhusu chaguzi yaku kusanya sampuli ya kizazi mwenyewe, nilitaka jua na nilihisi afueni. Baada yakujaribu chaguzi hiyo, naweza sema kwa kweli ilikuwa uzoefu chanya sana”.
Baada ya kuomba miadi na GP wake, uchunguzi ulikuwa rahisi.
“Walipitia mchakato wa uchunguzi wa kizazi nakunipa kifaa chakutumia. Maelezo kwenye kifaa hicho, yalikuwa rahisi sana kufuata.”
I think it's just the full privacy and control and not just being a passive patient that was big for me. Definitely there was very, very reduced stress.Jyotsna Oliver, health consumer
Kushinda vizuizi vya uchunguzi wa kizazi
Ina sisimua kudhani kuwa Australia inaweza kuwa nchi ya kwanza kuangamiza saratani ya kizazi.
Ila baadhi ya vizuizi vya lugha na utamaduni, vina sababisha uwepo wa viwango vya chini vya vipimo miongoni mwa wanawake kutoka jumuiya za tamaduni nyingi na Mataifa ya Kwanza.
Hata hivyo, shirika la Australian Multicultural Health Collaborative, lina fanya kazi kupiga jeki idadi ya wanawake wanao fanya vipimo katika jumuiya mpango wa FECCA.
Nidia Raya Martinez ni Meneja Mkuu wa Programu katika ushirikiano, yeye hufanya kazi na mashirika ya jumuiya kote nchini kuongeza viwango vya uchunguzi.
Inapokuja kwa swala la uchunguzi wa kizazi, wanawake kutoka mazingira ya jumuiya za tamaduni nyingi, wana achwa nyuma na haswa wanawake ambao ni wageni nchini, Bi Martinez amesema.

Own It Poster
Hiyo ndiyo sababu kifaa kipya chaku jifanyia kipimo kita badilisha hali ya sasa.
Kwa kuchukua udhibiti wa uchunguzi wao binafsi wa kizazi, wanawake hawata pitia uzoefu tena wa vizuizi ambavyo vinge wazuia kufanya vipimo ambavyo vina uwezekano waku okoa maisha yao.
“Bado inastahili fanywa ndani ya zahanati ya afya ila, unaweza enda nyuma ya pazia, vua nguo zako kwa faragha, chukua sampuli yako mwenyewe na kisha, irejeshe kwa daktari, au wakati mwengine wanaweza kwambie uende katika msalani kufanya kipimo hicho, kutegemea na zahanati ya afya unayo tembelea. Na hiyo ni chaguzi nzuri kwa wale ambao huenda hawajihisi starehe haswa, kama kuna daktari wa kiume anaye husika..”
Kufikisha taarifa ndani ya jumuiya
Shirika la The Collaborative limeshuhudia ongezeko la uchunguzi wa kizazi kupitia ushirikiano wao na mashirika ya jumuiya. Kupitia matukio ya jumuiya, wanawake wanachukua fursa kujielimisha nakuomba miadi ya uchunguzi, wakati mmoja kama kundi.
“Ila baadae pia kwa wale ambao wanapata taarifa, kisha wahisi starehe kuzungumza na daktari wao kuhusu uchunguzi, na pia nadhani kuzungumza nama rafiki wao na familia yao,” Bi Martinez amesema.
“Na wanaume kurejea nyumbani kwao nakupendekeza kwa wake, binti na mama zao kuwa pengine wanastahili fanya uchunguzi wa kizazi pia.”
Usi i ahirishe
Ni kawaida kwa watu kuchelewesha uchunguzi wao, Bi Oliver amesema. Ila, hakuna sababu nzuri yaku chelewesha uchunguzi huo.
“Jaribu chaguzi yaku kusanya sampuli mwenyewe. Nafsi yako ya usoni ita kushukuru.”
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia ya fafanuliwa, kwa habari muhimu zaidi na vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una swali lolote au wazo la mada? Tutumie barua pepe kwa: australiaexplained@sbs.com.au