Mazoezi hayo yameingia siku ya nne, wakati Taipei ikiishtumu Beijing kwakufanya matayarisho ya shambulizi kubwa.
Nayo Australia imejivuta katika mgogoro huo, balozi wa China mjini Canberra aki ikosoa vikali serikali ya shirikisho kwaku ikosoa Beijing kwa matumizi ya makombora aina ya ballistic karibu ya Taiwan.
Balozi wa China, Xiao Qian anatarajiwa kuhotubia mkutano wa waandishi wa habari wa taifa Jumanne 9 Agosti wiki ijayo.