Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia

250627 One millionth Event report_02.jpg

Credit: Credit: Department of Foreign Affairs and Trade

Australia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu lake kwa ukimbizi mkubwa wa dunia nzima.


Imekuwa zaidi ya miaka 25 tangu Tahera Nassrat alipo lazimika kutoroka Afghanistan.
Kwa kuogopa kuwa kazi yake na shirika la kimataifa ingeweza kumfanya kuwa shabaha kwa Taliban, alikimbilia Pakistan mwanzoni.

Niliona hofu sana, bila shaka. Kwa sababu mimi ni mwanamke, na ni kinyume na imani ya Taliban, kama wanawake Waislamu hamwezi kufanya kazi na wageni. Nililazimika kuacha familia, marafiki, nchi, kumbukumbu. Kila kitu mnachoamini kuwa ni chenu, mnalazimishwa kuacha. Niliondoka nchini si kwa hiari, bali kwa sababu nililazimika kuchukua uongozi wa maisha yangu tangu nikiwa mdogo sana.
Tahera Nassrat
Safari yake kama mkimbizi hatimaye ilimfikisha Australia, na sasa Tahera anaishi na kufanya kazi Parramatta huko Sydney Magharibi kama mhasibu wa kodi, na mkufunzi wa biashara. Yeye ndiye mwanzilishi wa Afghan Peace Foundation, shirika ambalo linatoa mwongozo wa kifedha na msaada wa ajira kwa wengine wenye asili ya wakimbizi.

Tunafanya kazi nyingi za ajira kwa wakimbizi ili kuwaunganisha na kazi. Bila shaka, wakimbizi wanapofika katika nchi mpya, wanakumbana na msongo mwingi. Jukumu langu ni kutoa elimu.
Tahera Nassrat
Yeye ni mmoja wa karibu watu milioni moja waliohamia Australia kupitia mpango wa wakimbizi na ubinadamu wa nchi hiyo tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti katika Baraza la Wakimbizi la Australia, Rebecca Eckart, anasema kuwa kibali cha kudumu cha ubinadamu cha milioni moja kinatarajiwa kutolewa karibuni.

Tunaamini kuwa takriban viza elfu tia tisini na nane zilitolewa hadi mwezi Juni mwaka huu. Kwa hivyo, tunatarajia kuwa katika miezi ijayo, viza ya milioni moja itatolewa. Hii ina maana kwamba kwa zaidi ya miaka themanini 80 iliyopita, watu waliokuja kupitia mpango wetu wa wakimbizi na kibinadamu wamewasili Australia
Bi. Eckart
 Katika miaka mitano baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Australia iliwakaribisha wakimbizi zaidi yaelfu mia moja sabini kutoka Ulaya. Vita vya Vietnam vilisababisha pia mwitiko mkubwa, na kulikuwa na makazi laki moja katika kipindi cha miaka 10.

Idadi ya mwaka ya wakimbizi iliongezwa hadi elfu ishirini na mbili katika miaka ya elfu moja mia tisa themanini na katika miaka ya elfu moja mia tisa tisini, viza mpya ya Msaada Maalumu ilianzishwa kutokana na migogoro katika maeneo kama Yugoslavia ya zamani, Timor ya Mashariki, Lebanon, na Sudan, miongoni mwa mengine. Kisha mkazo ulielekezwa kusaidia wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati, Afrika, na Asia-Pasific ikijumuisha kiasi maalumu cha kila mwaka , cha wakimbizi elfu kumi na mbili kutoka Syria na Iraq kuanzia mwaka wa elfu mbili na kumi na tano.

Bi. Eckart anasema kwamba tukikaribia viza yetu ya milioni moja ya kibinadamu ni ukumbusho wa hadithi mbalimbali za binafsi zinazounda historia hii.

Leo kuna mamilioni ya watu ambao wameunganishwa na mpango wetu wa kibinadamu, ama moja kwa moja au kupitia wazazi wao, babu na nyanya au mababu zao. Ni wakati wa kihistoria sana
Bi. Eckart

Profesa Daniel Ghezelbash [[gizz-ell-bash]] ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kaldor cha Sheria ya Wakimbizi wa Kimataifa. Anasema hatua hii pia inatoa fursa ya kutafakari jinsi Australia inavyoweza kuboresha mwitikio wake kwa makazi ya kimataifa.

Nafikiria ni sababu ya kusherehekea na wakati wa kuenzi mchango wa kubadilisha maisha ambao wakimbizi na familia zao wameufanya kwa jamii yetu, na uchumi wetu kwa miongo mingi sasa. Lakini pia kutumia wakati huu kutathmini upya ,baadhi ya njia zetu za sasa na kujaribu kurejea kwenye misingi yetu bora.
Proffesor Daniel Ghezelbash


Mpango wa kibinadamu wa Australia unajumuisha makundi mawili muhimu.

Kati ya mwaka 1947 na 2023 viza za kudumu nyingi zaidi - zaidi ya elfu mia nane Hamsini zilitolewa kwa wale waliotuma maombi ya ulinzi kutoka nje ya Australia. Zaidi ya viza elfu themanini na moja zilitolewa kwa wale waliosaka ulinzi baada ya kuwasili Australia. Profesa Ghezelbash anasema mtazamo wa Australia si thabiti.

 

Nadhani programu yetu ya makazi upya kwa ukarimu mkubwa , inapingana sana na jinsi tunavyowatendea watafuta hifadhi. Na hivyo, nadhani hapo ndipo matatizo makubwa na ukosoaji mkubwa wa sera zetu unatoka.
Professor Ghezelbash
 

Mnamo mwaka wa elfu mbili na moja, Australia ilianzisha sera ya usindikaji wa wakimbizi wanaowasili kwa mashua, na sheria ilibadilishwa mwaka elfu mbili kumi na tatu ili kuzuia wakimbizi wanaowasili kwa mashua wasipate visa za kudumu. Sera hii ya usindikaji nje ya nchi imeungwa mkono na pande zote za kisiasa tangu mwaka 2012 - lakini Profesa Ghezelbash anasema sera za wakimbizi za Australia zimekosolewa sana kimataifa.

 
Sera ya kuwarudisha wahamiaji baharini imefunga kabisa mawasiliano ya kutafuta hifadhi , kwa watu wanaowasili bila idhini, ambao ndio watu wanaohitaji zaidi ulinzi.Na hivyo sera hizi ni kinyume cha sheria za kimataifa na pia zina madhara makubwa kwa watu ambao zinalenga.
Professa Ghezelbash

Australia inapojiandaa kumkaribisha mkimbizi wake wa milioni moja kwa visa ya kudumu, wanasema kuna sababu ya kusherehekea pamoja na miito ya dharura kwa ajili ya mageuzi.


Nadhani tunapaswa kutafakari njia tunazoweza kupatanisha vyema wasiwasi kuhusu usalama wa mipaka, na kuwapa watu fursa ya ulinzi kwa kiwango kikubwa zaidi. Sera hizi zinatoa ishara mbaya kimataifa , na Australia inapaswa kuwa kiongozi kuhusiana na kukuza ulinzi, lakini kwa kweli, tumekuwa tukifanya kinyume kabisa, tukijenga mifano hii ya kurudishana ambayo imeigwa duniani kote.
Professor Ghezelbash
 

Bi Nassrat anasema kwamba kunahitajika mabadiliko katika simulizi, ili wale wanaotafuta ulinzi wasionekane tena kama tatizo la kisiasa.

 
Ninasikia watu wakisema 'oh, ninyi ni wakimbizi, daima ni mzigo kwa serikali.' Tuko hapa, tukikaa pamoja na ninyi mezani, tunachangia. Wakimbizi wanafika nchini kama Australia, kama wanavyofanya katika nchi nyingine yoyote, wakiwa na utamaduni tajiri, uwezo, na uwajibikaji. Wanataka kuchangia.
Bi. Nassrat

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service