Key Points
- Thousands of Indigenous children were force from their families and into white society.
- These removals caused deep, lasting trauma passed down through generations.
- Communities are healing through cultural reconnection and support programs.
- Education and national recognition are key to healing.
Onyo la maudhui: Makala haya yana nyenzo zaku kera, zinajumuisha marejeleo yakiwewe, kuondolewa kwa watoto na watu waki Aboriginal na wana viswa wa Torres Strait walio fariki wana tajwa.
Tangu 1910 hadi katika miaka ya 1970, maelfu ya watoto waki Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait wali ondolewa kwa utaratibu kutoka familia zao chini ya sera rasmi za serikali. Watoto hao waliwekwa ndani ya taasisi au katika familia zingine zisizo zawatu wa asili.
Kwa nini watoto wali chukuliwa?
Shannan Dodson, ni mwanamke wa ukoo wa Yawuru kutoka eneo la Broome yeye pia ni mkurugenzi mtendani wa shirika la Healing Foundation, amesema kulikuwa na kusudi lakuharibu nyuma yakuondolewa kwao.
“Kilicho vunja moyo kuhusu vizazi vilivyo ibiwa ni kwamba, ilikuwa makumi yama elfu ya watoto walio ondolewa, kwa sababu pekee yakutaka kuwa ingiza katika tamaduni isiyo yawa Aboriginal... Wengi wa watoto hao wali nyanyaswa na wengi wao, hawaku wahi ona familia zao tena.”
Watoto wali lengwa haswa kwa sababu, ilikuwa rahisi zaidi kwao kukubali wanavyo ambiwa na, kukana utamaduni wao. Mara nyingi familia zilidanganywa, zili ambiwa kuwa watoto wao walifariki au kwamba hawa takiwi
Utunzaji mubaya wa kumbukumbu, umefanya iwe vigumu kujua watoto wangapi wali chukuliwa ila, idadi hiyo inaweza kuwa mtoto mmoja kati ya watoto watatu. Hata hivyo, tunajua, kuwa kila jamii yawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait ilibadilishwa daima, na makovu bado yako.

CANBERRA, AUSTRALIA - FEBRUARY 13: Members of Australia's Stolen Generation react as they listen to Australian Prime Minister Kevin Rudd deliver an apolgy to indigenous people for past treatment on February 13, 2008 in Canberra, Australia. The apology was directed at tens of thousands of Aborigines who were forcibly taken from their families as children under now abandoned assimilation policies. (Photo by Mark Baker-Pool/Getty Images) Credit: Pool/Getty Images
Watoto wali enda wapi?
Watoto wengi walio ibiwa, walipelekwa katika taasisi za serikali na kanisa kote nchini.
Taasisi hizo zilijulikana kama vituo vya mafunzo au mabweni ambako watoto walikuwa chini ya nidhamu kali. Utambulisho wao uli ondolewa, na walipewa majina mapya, lugha na dini mpya.
Mara nyingi ndogu walitengwa, na baadhi ya taasisi zilitoa makaazi kwa watoto tu.
Mnamo 1943, akiwa na miaka minne, Aunty Lorraine Peeters, mwanamke wa ukoo wa Gamilaroi na Wailwan, alipelekewa katika nyumba ya mafunzo ya nyumbani ya wasichana waki Aboriginal ya Cootamundra jimboni NSW. Kaka zake wawili walipelekwa katika nyumba ya mafunzo yenye utata ya Kinchela Aboriginal Boys' Training Home.
“Adhabu ilikuwa lazima, ukisahau kuwa mzungu,” anakumbuka.
“Hatungeweza hata zungumza kuhusu kuwa mu Aboriginal. Na ukichukulia hilo kama mtoto mwenye miaka minne, ukioshwa akili. Punde unasahu tamaduni zaki Aboriginal na unajifunza tamaduni zawa zungu. Na adhabu ilikuwa mbaya katika sehemu hizo.”
Kwa miaka 10 iliyofuta Aunty Lorraine alipata mafunzo yakuwa mtumishi wa nyumbani kwa familia za wazungu.
Leo, yeye ni mtetezi mahiri wa wahanga, na ni mwanzilishi wa mradi wa Marumali, mpango wa uponyaji unao endana na mahitaji ya walio pitia uzoefu wakuondolewa kwa nguvu.

Shannan Dodson CEO Healing Foundation
Kiwewe cha vizazi ni nini?
Kiwewe ambacho watoto wanakabili, familia na jumuiya kina endelea kujirudia katika vizazi.
Leo kuna vijana ambao hawajijui, wanako toka au kwa nini wana tabia fulani, Aunty Lorraine amesema.
“Ni mzunguko mubaya. kama hautu uvunji katika familia zetu, ita endelea.”
Kwa sababu ya ukosefu wakihistoria wa mifumo ya usauidizi, kiwewe mara nyingi kime changiwa bila kujuwa kwa watoto, wanapo shuhudia uzoefu wa machungu wa waziwi wao nama babu zao.
Hali hii inajulikana kama kiwewe cha vizazi.
Wahanga huzungumza kuhusu jinsi inaweza kuwa vigumu kuwalea watoto wao, kwa sababu hawaku kuwia katika mazingira ya upendo nakusaidiwa, Shannan Dodson ame elezea.
“Baadhi ya wahanga wamekiri kuwa kwa sababu ya kiwewe walicho pitia, kwa masikitiko wame hamisha kiwewe hicho kwa watoto wao wenyewe. Na tuna ona mzunguko huo, ukijirudia kwa wajukuu na vitukuu. Na ndiyo sababu tuna iita ya vizazi.”
Dalili ya kiwewe cha vizazi inaweza onekana leo katika viwango vikubwa vya kuvunjika kwa familia, vurugu, kufungwa, matumizi mabaya ya mihadarati na vilevi pamoja na kesi zaku ji uwa.
Jamii sasa zina fanya juhudi yaku maliza mzunguko wa kiwewe kupitia uponyaji.

A vital component of healing is education—ensuring that all Australians understand the truth about the Stolen Generations. Credit: davidf/Getty Images
Kupona kiwewe kuna fanana je?
“Nadhani uponyaji ni kitu kinacho fanana tofauti kwa watu tofauti ila, tunajua kuwa wahanga wanahitaji ji amulia jinsi uponyaji huo unavyo fanana kwao,” Shannan Dodson amesema.
Kupona kuna maana yakujenga miundo yakifamilia na jamii imara. Ina maana pia yakujenga hali ya utambulisho na fahari. Kuunganishwa tena na ardhi, utamaduni na lugha, husaidia kurejesha utambulisho ulio potea.
Wahanga pia wame elezea mahitaji yao yakuchangia uzoefu wao na kuweza kuzungumza kwa uhuru kuhusu dhulma zakihistoria.
“Katika miduara na mikusanyiko, unatengeza uponyaji ufanyike hapo,” Aunty Lorraine amesema kuhusu kazi yake na shirika la Coota Girls Aboriginal Corporation, lililo anzishwa na wakaaji wazamani wa nyumba ya mafunzo ya Cootamundra.
“Wanazungumza kuihusu, wanapona kuipitia, kwa kuzungumza, kuchangia na jinsi wanavyo zidi kufanya hivyo, hawa sahau liki.”
Kibonzo cha kiwewe cha kizazi, Shirika la Uponyaji
Video hii ina sauti ya mtu aliye fariki.
Elimu na kusema ukweli
Sehemu nyingine muhimu ya uponyaji ni elimu, kuhakikisha kuwa wa Australia wote wana elewa ukweli kuhusu vizazi vilivyo ibiwa.
“Ningependa ona (wa Australia wasio wa asili) waki wapa watoto wao fursa yakujifunza historia ya kweli ya nchi hii.” Aunty Lorraine ame omba, “na kubomoa mifumo, kuibomoa nakuanza tena kwa sababu sera zilizo andikwa kuhusu watu wetu, niza ubaguzi wa rangi, kwa misingi ya ubaguzi wa rangi.”

Leilla Wenberg, a member of the Stolen Generation removed from her parents car at 6 months of age, holds a candle during a National Sorry Day commemorative event at the Royal Prince Alfred Hospital on May 26, 2009 in Sydney, Australia. National Sorry Day has been held annually on May 26 since 1998 to acknowledge the wrongs that were done to indigenous families of the stolen generation. Credit: Sergio Dionisio/Getty Images
Nini sasa kwa wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa?
Katika tukio muhimu mnamo 2008, Waziri Mkuu Kevin Rudd ali omba msamaha ulio kuwa ume subiriwa kwa muda mrefu kwa Vizazi vilivyo Ibiwa, wajukuu wao na familia zao.
Kilicho fuata ni mipango na maendeleo kadhaa yanayo jumuisha kuanzishwa kwa Shirika la Uponyaji.
Wahanga na familia zao, wanahitaji msaada endelevu, Shannan Dodson amesema.
“Shirika letu lina tetea mfuko wakitaifa wa uponyaji, kuhakikisha kuwa haki inayo salia inayo stahili patikana kwa wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa, inafanyika kabla wahanga wengine wafariki.”
Kupitia miradi kama Marumali, msaada kutoka shirika la Uponyaji na hatua zinazo ongozwa na jamii, uponyaji wa vizazi unaweza endelea.
Uponyaji wa kweli pia, unahitaji Australia kwa ujumla, iwasikize na iwasaidie wahanga kudai hadhithi zao.
READ MORE

What is Closing the Gap?
Jiandikishe au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Explained kwa taarifa za ziada na maelezo muhimu kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una maswali yoyote au mawazo ya mada? tutumie barua pepe kwa australiaexplained@sbs.com.au