Kanda hiyo ya jiji imefanya zaidi ya siku 100 ndani ya vizuizi. Idadi ya kesi zinapo endelea kupungua katika kanda ya Victoria, wakazi wame endelea kuregezewa vizuizi mbele ya jiji la Melbourne, na mageuzi ya ziada yanatarajiwa kutekelezwa.
Kuanzia usiku wa manane wa tarehe 18 Oktoba, vizuizi vya nyumbani katika maeneo yakanda vita futwa, na wakazi wataruhusiwa kuwapokea wageni wawili pamoja na watu ambao wako chini ya hifadhi yao kwa siku kutoka familia yoyote.
Kumbi zamigahawa katika maeneo ya kanda, zitaweza ongeza idadi ya watu wanao hudumiwa kufikia watu 70 katika maeneo ya nje, na idadi yawatu 40 katika maeneo ya ndani. Maktaba pamoja na maktaba zakuchezea nazo pia zitafunguliwa tena, wakati mikusanyiko yakidini katika sehemu za nje, itaongezeka kutoka idadi ya watu 20, na huduma za utalii zenye leseni zinazo tumia magari yaliyo wazi sehemu za juu nazo zinaruhusiwa kuanza oparesheni zao tena.
Mageuzi ya ziada yame ratibiwa kwa kanda ya Victoria kuanzia usiku wa manane wa tarehe mosi Novemba.
Kwa taarifa kuhusu mageuzi ambayo yamefanywa jimboni Victoria, tembelea tovuti hii: https://www.dhhs.vic.gov.au/summary-of-the-changes-to-restrictions-for-metropolitan-melbourne-and-regional-victoria
Na unaweza endelea kupata taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako, kwenye tovuti hii sbs.com.au/coronavirus