Wakazi wa Victoria wahamasishwa wavae barakoa, baada ya ongezeko yamaambukizi ya coronavirus

Watu wavaa barakoa mjini Melbourne

Watu wavaa barakoa mjini Melbourne Source: AAP

Afisa mkuu wa afya wa Victoria anawahamasisha watu wavae barakoa wakiwa nje, wakati jimbo hilo limerekodi visa vipya 288 vya COVID-19.


Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews naye amesema kuvaa barakoa kunaweza sababisha tofauti kubwa kwa viwango vya maambukizi.

Jimbo la Queensland lilifungua mipaka yake kwa kila mtu isipokuwa watu kutoka Victoria wakati, jimbo la Tasmania liliamua kuchelewesha kufungua mipaka yake hadi tarehe 31 Julai. Kiongozi wa jimbo hilo Peter Gutwein amesema, anawasiwasi kuhusu virusi hivyo kusambaa kisiwani humo kutoka bara.

Nalo jimbo la magharibi Australia limeamua kuchelewesha hatua zakuregeza vizuizi vya coronavirus hadi tarehe mosi Agosti.

Uamuzi huo umejiri baada ya zaidi ya idadi yawatu wa Victoria elfu moja, kuingia katika jimbo la W.A katika wiki iliyopita.

Na unaweza pata taarifa mpya kuhusu coronavirus katika lugha yako kwenye tovui hii: sbs.com.au/coronavirus


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Wakazi wa Victoria wahamasishwa wavae barakoa, baada ya ongezeko yamaambukizi ya coronavirus | SBS Swahili