Serikali ya Kenya imeongeza muda wa kutotoka nje usiku ndani ya nchi nzima kwa siku 30.
Amri hiyo, imewekwa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa COVID-19 nchini humo.
Wakati akilihutubia taifa kutoka ikulu ya Nairobi Jumamosi, Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa kulegeza masharti kwa asilimia 20, huenda kutapelekea maambukizi mapya 200,000 na vifo 30,000 ifikapo Disemba.
Rais hata hivyo, amesema amri hiyo itaanza kutekelezwa kati ya saa tatu usiku hadi za kumi alfajiri kuanzia Jumapili.
Share






