Viongozi wa chama cha upinzani wame apa kuendeleza maandamano pamoja na wafuasi wao hadi wakati makamishna wa tume ya uchaguzi watakapo jiuzulu.

Vyombo vya usalama vime jitahidi kudumisha utulivu katika maandamano hayo, hata hivyo mazingira ya maandamano hayo yame sababisha vyombo vya usalama kutumia vitoza machozi kuwatawanya waandamanaji.

Kwa uelewa zaidi wa swala hili, SBS Swahili ilizungumza na mwanasheria Steve Nyaribo Isinta, ambaye ni mmoja wa wanasheria wanao miliki shirika la sheria la Saende & Ochola mjini Nairobi Kenya.
Kwa Maelezo ya ziada kuhusu Bw Steve Nyaribo Isinta na kazi yake tembelea tovuti shirika lake:
www.saendeocholalaw.com
Share





