Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Bunge na mahakama za Kenya zitakubali ombi laku vunja tume ya IEBC?

Ajuza akwama katika maandamano dhidi ya IEBC
Ajuza akwama katika maandamano dhidi ya IEBC Source: Getty Images

Published

Updated

By SBS Swahili

Source: SBS



Share this with family and friends


Chama cha upinzani cha CORD, kime kuwa kikiongoza maandamano dhidi ya makamishna wa tume ya uchaguzi ya Kenya inayo julikana kwa ufipi kama IEBC. Makamishna hao wame kabiliwa na kashfa za ufisadi na upendeleo kwa chama tawala, hali ambayo imesababisha chama cha upinzani kutokuwa na imani kwa uwezo wa tume hiyo kuandaa uchaguzi ulio huru nawa haki mwaka kesho 2017.

Viongozi wa chama cha CORD, Raila Odinga na Moses Wetangula wakiongoza maandamano dhidi ya IEBC
Viongozi wa chama cha CORD, Raila Odinga na Moses Wetangula wakiongoza maandamano dhidi ya IEBC Source: EPA/DAI KUROKAWA
Wakenya wengi wanao ishi nchini Australia wame kuwa waki hofia usalama wa jamaa zao nchini Kenya, SBS Swahili ilizungumza na Mh. Isaiya Kabira, waziri wa Kenya nchini Australia ambaye alitueleza msimamo wa serikali kwa maandamano dhidi ya IEBC.
Balozi wa Kenya nchini Australia, Mh Isaiya Kabira ofisini
Balozi wa Kenya nchini Australia, Mh Isaiya Kabira ofisini Source: Kenya High Commission, Canberra

Mh. Kabiira alizungumzia pia uamuzi wa serikali ya Kenya kufunga kambi ya Umoja wa Mataifa ya Dadaab ambayo iko karibu na mpaka wa Kenya na Somalia. Serikali ya Kenya ime endelea kusisitiza kuwa walio fanya shambulizi lili sababisha maafa makubwa katika chuo cha Garissa walitoka katika kambi hiyo ya Dadaab. Hata hivyo, bado haija thibitishwa iwapo baadhi yawatu walio fanya shambulizi hilo ni wakimbizi kutoka kambi hiyo ya wakimbizi.

 


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now