Takwimu za hivi karibuni zime baini kuwa idadi ya vijana ambao hawana ajira ina endelea kuongezeka. Vijana wengi kutoka jumuiya zawa Afrika nchini Australia wamo katika takwimu hizo, licha yaku na ujuzi wa kazi zao pamoja naku hitimu kwa shahada na hata elimu ya juu. SBS Swahili ilizungumza na Bi Malkia na Imara ambao wame amua kuzindua biashara yao (Ubuntu Flair) baada yaku vunjwa moyo kwa muda mrefu kupita mchanganyiko wa ukosefu wa fursa huduma zinazo faa. Tembelea tovuti yao kwa maelezo ya ziada kuhusu biashara ambayo wame zindua: www.ubuntuflair.com
Share





