Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Australia Yafafanuliwa:Je magari ya umeme yanafaa nchini Australia?| Mafuta Yalengwa

Australia Explained – Fuel in Focus

It is estimated that drivers can save up to 70 per cent on fuel and 40 per cent on servicing costs annually. Source: Moment RF / Tashdique Mehtaj Ahmed/Getty Images

Magari ya umeme (EV) yanazidi kuwa ya kawaida barabarani nchini Australia, wakati bei za mafuta ziki endelea kuto tabirika na madereva wengi zaidi wanatafuta njia za usafiri za bei nafuu. Haya ndiyo unayohitaji kujua kama unafikiria kuanza kutumia gari la umeme.


Published

By Zoe Thomaidou

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Magari ya umeme (EV) yanazidi kuwa ya kawaida barabarani nchini Australia, wakati bei za mafuta ziki endelea kuto tabirika na madereva wengi zaidi wanatafuta njia za usafiri za bei nafuu. Haya ndiyo unayohitaji kujua kama unafikiria kuanza kutumia gari la umeme.


Data ya tasnia inaonyesha idadi ya magari ya umeme ni takriban moja kati ya magari sita mapya yaliyo uzwa nchini Australia katika mwezi wa April 2026. Ila wakati mauzo yana ongezeka, maswali yana salia kuhusu bei nafuu, kuchaji na kama magari ya EV yanafaa kwa mazingira ya kuendesha magari nchini Australia.

Gari la umeme lina gharimu pesa ngapi nchini Australia?

Magari ya umeme bado yanagharimu zaidi wakati waku nunua kuliko magari ya petroli au dizeli, ingawa bei zimeshuka kadri matumizi na uchaguzi unavyoongezeka.

Hussein Dia, ni Profesa wa Teknolojia ya Usafiri na Uendelevu katika Chuo cha Teknolojia cha Swinburne. Anasema aina nyingi za bei nafuu zina patikana sasa.

"Miaka mitatu, minne iliyopita, tulikuwa na shida kupata gari la EV kwa chini ya $50,000. Siku hizi ziko katika kiwango cha kati cha elfu 30 na kwa motisha za serikali pia, zinaweza kuwa nafuu zaidi."

Madereva pia wanaweza kustahiki kupata motisha za serikali kulingana na mahali wanapoishi.

Wafanyakazi walio katika mpangilio wa kupunguza ushuru wa mishahara, wanaweza pata punguzo la kodi kwa kukodisha gari la umeme.

Alex Forrest, ni Meneja wa Magari na Mafuta katika shirika la Royal Automobile Club la Magharibi Australia. Ana elezea zaidi hapa:

“Kama una mkataba mpya wa kukodisha, unaweza pata punguzo la kodi ya faida za ziada. Kwa hivyo hiyo inaweza kuokolea maelfu ya dola kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ya kukodisha...”

Je ni bei nafuu kuendesha gari la umeme?

Ikilinganishwa na magari ya petroli na dizeli, magari ya umeme ni ya bei nafuu kuyaendesha.

Inakadiriwa kuwa madereva wanaweza okoa hadi asilimia 70 kwa mafuta na asilimia 40 kwa gharama za huduma kila mwaka.

Profesa Dia anasema gharama za chini za umeme na huduma zinaweza kuongezeka baada ya muda.

Umeme ni bei nafuu zaidi kuliko petroli kwa kilomita. Hatuhitaji kutegemea kuuagiza kama tunavyofanya na petroli. Na magari ya umeme, kwa sababu ni rahisi zaidi kimakanika, gharama za huduma pia ni za chini.
Hussein Dia

Kuchaji EV nyumbani kwa ujumla ni nafuu zaidi kuliko kutumia vituo vya kuchaji vya umma, kwa hivyo akiba ya jumla ya gharama ya uendeshaji inaweza kuwa ya chini kwa madereva ambao hutegemea sana kuchaji kwa umma.

Magari ya umeme yanaweza safiri umbali gani?

Profesa Dia anasema aina nyingi ya magari ya umeme sasa yanaweza kusafiri kati ya kilomita 400 na 500 kwa chaji moja.

Lakini usafiri wa masafa marefu bado unaweza kuhitaji mipango.

"Pale yanaposhindwa ni unapohitaji kusafiri kati ya majimbo... hasa katika maeneo ya kikanda. Kuna maelfu ya kilomita bila chaji za haraka."

Unaweza chaji gari la umeme nyumbani?

Wamiliki wengi wa EV huchaji magari yao nyumbani, kwa kutumia soketi ya kawaida ya umeme.

Alex Forrest anasema hii inaweza kuwafaa watu wanaoendesha magari umbali mfupi kila siku.

"Ikiwa una maegesho nje ya barabara na sehemu ya umeme katika gereji au eneo la maegesho, unaweza kuichaji kwa kutumia kebo hiyo ya umeme."

Madereva wanaosafiri umbali mrefu wanaweza kufaidika kwa kuweka chaja maalum nyumbani.

Kama utalazimika kuendesha gari mbali zaidi kila siku, fanya safari ndefu na utumie nguvu zaidi ya betri... hapo ndipo chaja ya nyumbani ina hitajika.
Alex Forrest

Watu wanaoishi katika magorofa wanaweza hitaji idhini kutoka kwa wasimamizi wa jengo hilo kabla ya kuweka chaja maalum ya EV.

Unastahili jua nini kabla ya kununua EV iliyo tumiwa?

Soko la magari ya umeme yaliyotumika nchini Australia bado ni jipya, lakini imani ya watumiaji katika magari ya umeme yaliyotumika inaongezeka.

Wataalamu wanapendekeza kuangalia udhamini wa betri, chaguzi za huduma na usaidizi wa baada ya mauzo kabla ya kununua.

Bw. Forrest anasema watumiaji wanapaswa kutafiti uzoefu wa umiliki pamoja na tathmini ya magari.

"Kufanya utafiti wako, si tu mapitio ya magari, bali pia kujua watu wanafikiria nini kuhusu uzoefu wa umiliki ni kama... kuhakikisha unajua hasa unachopata kwa bei unayotaka kulipa, na kwamba inakidhi mahitaji yako pia."

Jisajili au fuata podikasti ya Australia Yafafanuliwa kwa taarifa na vidokezo muhimu zaidi kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Je una maswali au mawazo ya mada? Tuma barua pepe australiaexplained@sbs.com.au


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now