Mkutano huo uliandaliwa siku chache baada ya serikali ya New South Wales kuondoa vizuizi dhidi ya mikusanyiko katika sehemu za ibada kote jimboni, hatua ambayo iliwaruhusu waumini wengi kujumuika pamoja tena baada ya mwaka mzima wakushiriki ibada nyumbani.
Askofu Peter Rwagasore, ali alikwa kuongoza ibada hiyo ya pasaka na katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifafanua maana na umuhimu wa maadhimisho ya Pasaka kwa waumini.