Majukwaa yakiasili kama National Indigenous Television (NITV) na mitandao yakijamii inavunja vizuizi, kuwezesha sauti zawa Australia wa Kwanza na kukuza uelewa unao jumuishi zaidi wa utambulisho wakitamaduni tofauti wa Australia.
Kujifunza kuhusu mabadiliko haya hutoa ufahamu wa thamani kwa historia ya kweli ya nchi hii, safari yake kuelekea usawa na tamaduni Tajiri zinazo unda misingi ya Australia ya kisasa.
Kuelewa mitazama yawa Australia wa Asili ni hatua muhimu pia kuelekea kuwa na uhusiano wa heshima na kuchangia kujumuishwa.
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia ya fafanuliwa, kwa habari muhimu zaidi na vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una swali lolote au wazo la mada? Tutumie barua pepe kwa: australiaexplained@sbs.com.au