Huna haja ya kupitia katika mfumo wa sheria peke yako. Nchini Australia, huduma za kisheria za bure zipo kwa ajili yakuwatetea wanawake walio katika mazingira magumu kwa njia salama, za siri na zinazofaa kitamaduni.
Mfumo wa kisheria wa Australia unaweza kuwa mgumu kuupitia. Kwa wanawake, changamoto zinaongezeka. Sio tu kwamba wana uwezekano mkubwa wa kuhitaji usaidizi wa kisheria, lakini pia wanakabiliwa na vikwazo zaidi vya kufikia msaada huo.
Kukabiliana na changamoto hizi, huduma maalum za kisheria za wanawake zinahakikisha kwamba wanawake wanaweza pata usaidizi wanapo uhitaji zaidi.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





