Australia yafafanuliwa: mkutano wa G20 umekamilika

G20 Summit

Australia's Prime Minister Anthony Albanese (R) during the opening plenary session at the G20 Summit in Johannesburg, South Africa. Picture date: Saturday November 22, 2025.. Source: AAP / Leon Neal/PA Wire

Viongozi wa dunia wamesifu mkutano wa kwanza wa G20 kufanyika Afrika kama ushindi kwa ushirikiano wa kimataifa, hata walipokuwa wakizungumzia changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usawa na vita, dhidi ya muktadha wa ushindani unaobadilika wa kidiplomasia. Kutokuwepo kwa Rais Donald Trump kumewafanya watu kujiuliza maswali kuhusu nafasi ya Marekani katika mpangilio wa dunia unaobadilika.


Mkutano wa kwanza wa kilele wa G-20 kufanyika katika bara la Afrika umemalizika. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepongeza mkutano wa viongozi wa uchumi mkuu wa dunia kama ushindi wa ushirikiano wa kimataifa - pamoja na kupata makubaliano kutoka kwa wengi wao juu ya tamko la pamoja.

Tamko la viongozi wa mkutano wa G20 Afrika Kusini ni zaidi ya maneno. Ni ahadi ya kuchukua hatua halisi ambazo zitaboresha maisha ya watu kila sehemu ya dunia. Zaidi ya hayo, inathibitisha upya ahadi yetu kwa ushirikiano wa kimataifa na utambuzi wetu kwamba malengo yetu ya pamoja ni muhimu zaidi kuliko tofauti zetu.
Cyril Ramaphosa

Lakini kulikuwa na upungufu mmoja. Marekani iligomea mkutano huo, ikitaja madai ambayo yamekataliwa kwa upana kwamba wachache wa jamii ya wazungu wa Afrika Kusini wananyanyaswa. Serikali ya Rais Trump pia ilikosoa tamko la pamoja, hasa kwa kipaumbele chake kama ushirikiano katika biashara na mazingira.

 Kutokuwepo kwao kulipokelewa kwa hisia mchanganyiko kwenye mkutano huo, na baadhi ya viongozi kama Waziri Mkuu wa Kanada, Mark Carney, wakibainisha umuhimu unaoongezeka wa uchumi unaoibukia kutoka Afrika, Asia na Amerika ya Kusini. Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva alisema mtindo wa Rais Donald Trump wa kufanya mambo bila ushirikiano unaweza kuthibitika kuwa mbaya.

 
Rais Trump amekuwa akionyesha hili kwa miezi kadhaa sasa. Tayari ameondoka kutoka UNESCO na Shirika la Biashara la Dunia. Anajaribu kuhubiri mwisho wa ushirikiano wa kimataifa kwa vitendo, akijaribu kuimarisha kujitenga. Ninaamini ushirikiano wa kimataifa utashinda ... Ikiwa yeyote alikuwa na mawazo kwamba wanaweza kudhoofisha ushirikiano wa kimataifa, matukio haya, COP na G20 hapa Afrika Kusini, yanaonyesha kwamba ushirikiano wa kimataifa zaidi ya kuwa uhai.
Lula da Silva
 
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alionya kwa mafumbo kwamba "G20 inaweza kufikia mwisho wa mzunguko." Lakini maoni ya Rais wa Brazil yalishirikiwa na kiongozi wa uchumi mkubwa zaidi wa Ulaya - Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz

Ninahisi kusema kwamba jambo lililonigusa sana hapa, na ambalo naliona ni la kuvutia, ni ukweli kwamba tunaweza kuona kuwa dunia kwa sasa inapitia mpangilio upya na muunganiko mpya unajengwa hapa, na kwamba Marekani imecheza jukumu dogo sana. Sidhani ilikuwa uamuzi mzuri kwa serikali ya Marekani kutokuwepo hapa. Lakini serikali ya Marekani inapaswa kujiamulia yenyewe. Ilikuwa vizuri kwetu kuwa hapa.
Friedrich
Mwishoni, nchi zote zilizo hudhuria zilikubali tangazo la pamoja, isipokuwa Argentina ambayo haikukubaliana na uundaji wake wa mgogoro wa Mashariki ya Kati. Tamko hilo linasisitiza uzito wa mabadiliko ya hali ya hewa na linataka hatua zaidi za muendelezo, likisifia malengo ya kijasiri ya kuongeza nishati mbadala. Lakini limekosolewa kwa kushindwa kuelezea majukumu ya kuondoa mafuta ya kisukuku.

Pia linazingatia usawa wa kimataifa, likibainisha gharama ya adhabu ya kuhudumia deni, ambayo inawakumba nchi masikini. Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, alihutubia mkutano huo, akisema kuwa hatua za angahewa zinaweza kufikiwa kwa ukuaji wa uchumi.

Ujumbe muhimu ambao lazima tufikishe ulimwenguni kuhusu hatua za mabadiliko ya tabianchi si suala la kuomba taifa lolote kutupilia mbali kazi, ustawi au usalama ambao watu wake wanastahili. Ni kuhusu kufanya kazi na kila taifa kuimarisha kizazi kijacho cha ukuaji wa kiuchumi huku tukilinda mazingira kwa vizazi vijavyo.
Antony Albanese
Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alizungumzia Mpango wa Global Gateway wa Ulaya. Huu ni mradi wa miundombinu wenye thamani ya euro bilioni mia moja hamsini kwa Afrika, ambapo robo moja itaelekezwa kwenye mitandao na viunganishi ili kuharakisha mpito kuelekea kwenye nishati jadidifu.

 
Katika uwekezaji wa dola trilioni 2 katika nishati safi duniani mwaka jana, ni asilimia 2 tu ndiyo iliyoekezwa Afrika. Wakati huo huo, Afrika ina watu milioni 600 ambao hawana umeme na ni bara lenye uwezo bora zaidi wa nishati ya jua kwa asilimia sitini duniani. Hali hii haiwezi kuendelea
Ursula von der Leyen
Mkutano wa mwaka ujao utaandaliwa na Marekani, ambapo Rais Trump amesema anapanga kuufanya katika uwanja wake wa gofu huko Florida. Hii ilifanya kutokuwapo kwa Marekani kuonekana zaidi katika sherehe za kufunga mwaka huu, ambapo kiongozi wa nchi mwenyeji kawaida hukabidhi kwa mwenyeji mpya.

Hilo halikutokea, Cyril Ramaphosa akikataa kukutana na mwanadiplomasia ambaye alitumwa na Marekani badala ya Rais. Mchambuzi wa siasa za Afrika Kusini Oscar van Heerden kutoka the Mapungubwe Institute for Strategic Reflection, ambaye alihudhuria mkutano huo, anasema haina umuhimu.

Sio kuhusu utu wa Ramaphosa na Trump. Viongozi wengi walio hapa kwenye mkutano huu wanakubaliana na tamko hili, na hiyo ndiyo yote, basi. Nchi moja iliamua kususia, ni bahati mbaya kwamba tulitaka nchi hiyo iwepo lakini haipo. Lakini hii haimaanishi au kupendekeza kuwa kuna tatizo na tamko hili
Oscar van Heerden
 

Sanusha Naidoo, kutoka Taasisi ya Afrika Kusini ya Mazungumzo ya Ulimwengu anasema kwamba kutokuwepo kwa Bwana Trump kulikuwa kukosa heshima, lakini mwishowe, si jambo linalopunguza mafanikio ya mkutano huo.

 
Nadhani mwishowe mnajua kutokuwepo hapa kwao (Marekani) kunafungua viwango vya udhaifu, lakini pia kinaashiria kwamba kwa kufanya kile walichofanya, wamefungua mlango kwa tabia ya aina hiyo. Na nadhani hasira kutoka kwa baadhi ya viongozi wa G20 ilikuwa kwamba hatutadharirika kwa njia hii. Na kwa hivyo ukweli kwamba Marekani haipo hapa, haimaanishi kwamba wanakuwa wasio na umuhimu, lakini inamaanisha kwamba dunia inaendelea bila wao.
Sanusha Naidoo
 


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service