Burundi ya imarisha juhudi za kufikia usawa wa jinsia
Wikipedia / Public Domain Source: Wikipedia / Public Domain
Ulimwengu unaadhimisha hii leo tarehe 8 machi Siku ya Wanawake Duniani. Kauli mbiu ya maadhimisho mwaka huu ni " Imarisha Juhudi za Kufikia Usawa wa Jinsia.Burundi ni moja ya nchi zinazojivunia kuongeza usawa wa jinsia, hasa katika uwanja wa siasa baada ya kuwapa wanawake kwa uchache uwakilishi wa asilimia 30 kwenye taasisi za uongozi wa taifa. Hata hivo changamoto kubwa ni kumstaawisha mwaaamke wa Kijijini na yule mwenye kipato cha chini ambao wamezongwa na umaskini, kama anavyosimulia Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga katika makala haya kutoka Bujumbura, Burundi.
Share