Hivi karibuni Bw Mwita alikuwa miongoni mwa waigizaji walio igiza katika tamthilia ya Stateless, iliyo mulika maisha ya wakimbizi na waomba hifadhi ndani ya vizuizi vya uhamiaji vya Australia..
Tamthilia hiyo ilioneshwa kwenye runinga ya ABC na mtandao wa Netflix nchini Australia, ambako wapenzi wengi wa tamthilia wame itazama nakushiriki katika mijadala kadhaa iliyo ibuka.
Bw Mwita ali eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS pia, matumaini yake kwa sekta ya uigizaji nchini Tanzania, na mageuzi ambayo angependa kuona katika sekta hiyo ili iweze kuwa bora zaidi. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.