Mradi wa uhamiaji wa waziri mkuu wa Australia, pamoja na sera ya nishati mara nyingine zilikuwa kwenye ajenda ya kampeni.
Na katika taarifa zingine, mawaziri wa nishati wa mikoa na majimbo, watakutana mwezi ujao kushauriana kuhusu msimamo wao, kwa sera ya dhamana ya nishati ya taifa toka kwa serikali ya mseto.
Mawaziri hao hawatakuwa na uhaba wa vitu vyakusoma kabla ya mkutano huo kwa mfano; ripoti tatu muhimu zime tolewa kuhusu nishati, pamoja na uchunguzi ulio fanywa na serikali.





