Katika sensa za kabla, wafanyakazi kutoka ofisi ya takwimu ya Australia, walibisha hodi katika kila nyumba kufanya zoezi hilo. Ila janga la COVID-19 lime lazimisha zoezi hilo kufanywa katika hali tofauti kabisa.
Bw Claude ni afisa kutoka shirika la IMS katika kanda ya Illawarra, jimboni NSW. Shirika la IMS hutoa huduma mbali mbali kwa jamii zawahamiaji na wakimbizi wanao ishi katika maeneo ya Wollongong. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Claude aliweka wazi jinsi shirika lake pamoja na mashirika mengine kandani, yanavyo wasaidia wateja wao kushiriki katika zoezi hili la Sensa, wakati wana endelea kuzingatia masharti na vizuizi vyaku kabiliana na usambaaji wa maambukizi ya Coronavirus ndani ya jamii.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.