Rais Samia ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Afrika Mashariki kuwa Rais. Alijipata katika wadhifa huo, baada ya mtangulizi wake Dr John Pombe Joseph Magufuli kufia madarakani.
Licha ya Rais samia kuwa sehemu muhimu ya uongozi wa hayati Magufuli, baadhi yawatu walihoji uwezo wa mwanamke kuongoza taifa. Dkt Casta Tungaraza ni mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mahusiano kati ya Australia na Afrika (AGAAR).
Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Dkt Tungaraza alizungumzia changamoto ambazo wanawake hukabiliana nazo katika nafasi za uongozi, pamoja na afya ya mahusiano kati ya Australia na Tanzania baada ya mageuzi ya uongozi.