Ripoti yenye matokeo namapendekezo ya utafiti huo, ilizinduliwa hivi karibuni katika ukumbi wa chuo cha Western Sydney jijini Liverpoll, New South Wales, Australia.
Bi Eve ni mfanyakazi wa huduma ya jamii katika shirika la GLAPD, katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifunguka kuhusu baadhi ya mapendekezo ya ripoti hiyo, pamoja nakuhamasisha jamii iwalinde watoto dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani.