Licha yakuwa mbali, wengi wao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo yaliyo kuwa yakifanyika nchini kwao, kwa kasi isiyo yakawaida. Na katika muda wa miaka mitano ya uongozi wa hayati Dkt Magufuli, nchi hiyo ilikuwa imebadilika sana.
Bi Halima ni mweka hazina wa jamii yawatanzania, wanao ishi jimboni New South Wales. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alizungumzia hatua ambazo serikali ilikuwa imechukua, kuweka taifa hilo la Afrika Mashariki katika hatua bora miongoni mwa mataifa mengine yanayo endelea.
Bofya hapo juu usikize taarifa kamili.